Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa arithi mikoba kuongoza KNCU

10091 Kncu+pic TZW

Tue, 26 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Profesa John Boshe aliyewahi kuwa mhadhiri wa vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi katika masuala ya mazingira, amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Chama Kikuu cha Ushirika Kilimanjaro (KNCU).

Uchaguzi wake umekuja wakati KNCU kikijitahidi kujinasua na hali mbaya ya kifedha wakati huo huo kikijitahidi kuinusuru benki yake ya Ushirika (KCBL) isifungwe na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Profesa Boshe aliyewahi kuwa mhadhiri Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (Sua) na vyuo vingine vya masuala ya uhifadhi wa maliasili Cameroon, Japan na Marekani, anachukua nafasi ya Aloyce Kitau.

Mara baada ya kuchaguliwa katika mkutano mkuu maalum, Profesa Boshe aliamua kutema cheche aliposema kamwe hatashiriki wala kuunga mkono au kupitisha azimio la kuuza mali za chama.

Kauli ya Profesa Bee imekuja wakati KNCU ikiwa imeshauza shamba lake la Garagarua lenye ukubwa wa ekari 3,429 kwa Sh9.3 bilioni kulipa madeni likiwemo deni la Sh5.2 bilioni la Benki ya CRDB.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz