Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa Mbarawa: Tutachimba visima vinne mji wa Mlowe

78463 Pic+mbarawa

Fri, 4 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Waziri wa Maji nchini Tanzania, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali itachimba visima virefu vinne katika mji wa Mlowe mkoani Songwe ili kutatua changamoto ya maji inayowakabili wananchi wa eneo hilo.

Amesema awali walijenga mradi wa maji uliogharimu Sh556 milioni lakini baada ya kukamilisha haujasaidia kumaliza kero ya huduma hiyo.

Akizungumza leo Ijumaa Oktoba 4, 2019 katika ziara ya siku tatu ya Rais wa Tanzania, John Magufuli mkoani Songwe, Mbarawa amesema wanatarajia kuchimba visima virefu vinne na kujenga matenki ya kuhifadhi maji.

 “Kwa kufanya hivi tutamaliza kero kubwa ya maji kwenye eneo hili kwa sababu hakuna chanzo kingine tunachoweza kukitumia kuleta maji hapa,” amesema kiongozi huyo.

Kwa upande wake Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo amesema wamefanikiwa kujenga miundombinu mbalimbali kwenye miradi ya afya na elimu ikiwamo hospitali tatu.

Rais Magufuli amesema Serikali itaendelea kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz