Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prof Kitila ahoji kutokujengwa baadhi ya barabara Ubungo

KM Prof.Alexander Kitila Mkumbo

Fri, 11 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo amehoji juu ya barabara ya Kimara, Mavurunza na Kinyerezi (Kikwete Highway) iliyoahidiwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete 2010.

Akiuliza swali la nyongeza bungeni kwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Prof. Kitila amesema barabara hizo zilitolewa ahadi na Rais wa awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi Mhandi Godfrey Kasekenya amesema ahadi zote zinazotolewa na Viongozi wakiwemo Viongozi wakuu wa nchi zimekuwa zikitekelezwa.

Amesema kuwa barabara zote zilizozungumziwa na Mbunge Prof. Kitila Mkumbo zitajengwa kwa kiwango cha lami kadiri fedha itakavyopatikana.

Amesema umuhimu wa barabara hizo umeongezeka ikiwemo ya Kinyerezi inayofahamika kama Kikwete Highway kutokana na ujenzi wa kituo cha mabasi cha Kinyerezi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live