Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yatoa taarifa vifo vya watu 20 ajali ya Kahama

C05c0987 7095 4bf7 8cbd 4aff85466e84 Polisi yatoa taarifa vifo vya watu 20 ajali ya Kahama

Tue, 9 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu 20 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha magari manne ikiwemo treka wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Ajali hiyo imetokea katika barabara ya Isaka kwenye kijiji cha Mwakata halmashauri ya Msalala.

Ajali hiyo imetokea jana Agosti 8 majira ya saa 4 usiku ikihusisha gari ndogo aina ya IST (T880 DUE), Hiace (T350 BDX), lori (T658 DUW) na trekta.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali, inadaiwa kuwa trekta hilo lilikuwa likiendeshwa bila kuwa na taa za tahadhari (hazard) na kusababisha kugongana na uso kwa uso na Hiace.

Afisa muuguzi wa hospitali ya manispaa ya Kahama, Wilbert Mollel amesema kuwa jumla ya maiti 20 zimepokelewa sambamba na majeruhi 15.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani Shinyanga ambaye ni kamanda wa Polisi Mkoani Geita ACP Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa dereva wa trekta ambaye ni chanzo cha ajali amekimbia na juhudi za kumsaka zinaendlea.

Aidha Uongozi wa Mkoa wa Shinyanga ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Sophia Mjema umefika eneo la tukio na kulitaka jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kusimamia sheria ili kuepukana na vifo vinavyoepukika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live