Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yatoa huduma za matibabu kwa Wazee

Image 132 1140x640.png Polisi yatoa huduma za matibabu kwa Wazee

Fri, 9 Dec 2022 Chanzo: dar24.com

Jeshi la Polisi la Mkoa wa Arusha limetoa huduma ya matibabu na ushauri wa kiafya katika kituo maalumu cha uleaji wa wazee wanaoishi katika mazingira magumu,AST, cha jijini Arusha.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha (TPF NET), Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mary Kipesha amesema msaada huo wa vitu mbalimbali umeendana na huduma za zafya katika mwendelezo wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Amesema, mbali na kutoa msaada huo, katika siku hizo 16 za kupinga ukatili amebainisha kuwa wametoa elimu katika shule, hospitali, nyumba za ibada, masoko pamoja na stendi za mabasi ambapo jamii imepata uelewa wa kutosha.

Awali, Mkurugenzi wa Kituo hicho, Bi. Ester Njau amelishukuru Jeshi hilo kwa kutoa matibabu kwa wazee wanaoishi katika kituo hicho ambapo amebainisha kuwa matibabu hayo pamoja na vitu mbalimbali vilivyotolewa vitaboresha afya za wazee hao.

Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Elerai Bwana Losioki laizer ameshukuru Jeshi la Polisi kwa kuwajali wazee wanaoishi katika mazingira magumu na kutoa wito kwa makundi mengine kuiga mfano ulioneshwa na Jeshi

Chanzo: dar24.com