Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yataja 12 waliofariki ajali ya Lindi

Ajali Majeruhiiiiiiiiii.png Polisi yataja 12 waliofariki ajali ya Lindi

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JESHI la Polisi Mkoa wa Lindi limetaja majina ya watu 12 kati ya 15 waliokufa katika ajali ya basi la Baraka Classic Novemba 26, mwaka huu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi, John Iromi alilieleza HabariLEO kuwa basi hilo lenye namba za usajili T336 DPW liliacha njia saa 1:30 asubuhi na kugonga kingo ya barabara na kupinduka.

Kamanda Iromi alisema ofisini kwake kuwa ajali hiyo ilitokea katika maeneo ya kona ya Mputo Kata ya Mtama, Tarafa ya Mtama katika barabara ya Newala- Mtama katika Halmashauri ya Mtama wilayani Lindi.

Kamanda Iromi alimtaja dereva wa basi hilo ni Mohamed Omari (45) mkazi wa Mbagala, Dar es Salaam na akasema kijana huyo ni miongoni mwa waliopoteza maisha katika ajali hiyo. -

Kamanda Iromi aliwataja marehemu waliotambuliwa ni Adam Mmkoto (30) mkazi wa Dar es Salaam, Fatuma Bakari (miezi minane) mkazi wa Newala, Kassim Mussa (43) na Shaibu Mtalisi (58) mkazi wa Kitangali.

Marehemu wengine ni Afingwalu Kazumari (17) mkazi wa Newala, Aziza Selemani (16) mkazi wa Newala, Azizi Omari (35) mkazi wa Kitangali na Sumaiya Jafari (4) mkazi wa Newala.

Wengine ni Farihiya Abdala (3.5) mkazi wa Chaume Tandahimba, Albano Lipupa (28) mkazi wa Newala na Hakika Malasi (50) mkazi wa Newala.

Kamanda Iromi amesema majeruhi 20 kati ya 26 walipata tiba katika hospitali ya Nyangao katika Halmashauri ya Mtama na wameruhusiwa.

Ametaja majeruhi sita waliolazwa hospitalini hapo ni Jasmine Bakari (15), Arafa Mashuhuri (43), Swahiba Mohammed (17), Sophia Said (23), Zamda Rashid (47) na Yasin Jafari (30).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live