Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yamshikilia mlinzi anaedaiwa kuua Mwananchi kwa risasi

Polisi Ajiua Baada Ya Kumpiga Risasi Mkewe Polisi yamshikilia mlinzi anaedaiwa kuua Mwananchi kwa risasi

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mlinzi wa Hospitali ya Challote inayomilikiwa na Masista wa Kanisa Katoliki Wilaya ya Siha kwa madai ya kumuua kwa risasi mkazi wa Kitongoji cha Kilari, wilayani humo Nicholous Nzota (35-40).

Mkuu wa Wilaya ya Siha, Dk Christopher Timbuka amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo amesema limetokea saa moja usiku, Oktoba 1, 2023 katika eneo la hospitali hiyo huku akisema chanzo ni baada ya walinzi hao kuwashikilia mateka wanawake wawili waliowakuta mpakani wa eneo la hospitali hiyo jambo ambalo lilileta vurugu baina ya wananchi na walinzi hao.

"Ni kweli jana saa moja usiku kulitokea tukio la mauaji katika Kitongoji cha Kilari, kuna bwana mmoja alipigwa risasi na mlinzi wa Hospitali ya Challote ambapo chanzo ni ugomvi uliotokea baada ya walinzi kuwashikilia mateka wanawake wawili waliokutwa mpakani mwa eneo la hospitali," amesema Dk Timbuka.

Alipotafutwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Yahaya Mdogo, amesema Jeshi la Polisi linamshikilia mlinzi huyo kwa mahojiano zaidi juu ya tukio hilo.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Siha kwa taratibu nyingine zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live