Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yakanusha kutokea kwa ajali Kimara

Moto Kanusho Poilisi Kimara Ahjali (600 X 357) Polisi yakanusha kutokea kwa ajali Kimara

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dares Salaam limetoa ufafanuzi wa uzushi wa taarifa na kipande cha picha "clip" inayosambazwa kuhusu ajali inayotajwa kutokea katikati ya Kimara Stop over na Suka eneo la garage ikihusisha basi linalotokea Dodoma na Lori la cement kugongana uso kwa uso na magari yote kuungua moto.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Muliro Jumanne amesema “Taarifa hizo sio za kweli, zipuuzwe na tarehe ya leo 31.10.22, hata baada ya kupitia kumbukumbu zetu za mwaka huu 2022 hakuna ajali Iliyotokea eneo hilo ya namna hiyo”

“Taarifa hizo zina lengo la kuzua hofu na taharuki kwa Wananchi, hali hiyo haikubaliki, Jeshi la Polisi litachukua hatua za kisheria kwa aliyeanzisha kusambaza taarifa hizi hivi karibuni kwani inaonesha lengo ni kuzusha taharuki na hofu kwa Wananchi”

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dares Salaam linatahadharisha Wananchi kuacha kuzisambaza picha na taarifa hizo”

“Hali ya usalama Dar es Salaam imeimarishwa kwa kiwango cha juu na eneo la Kimara hakuna tukio la ajali iliyotokea kama taarifa hiyo inavyosema”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live