Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yakana kumkamata mwanafunzi Udom, chuoni haonekani

92737 Udom+pic Polisi yakana kumkamata mwanafunzi Udom, chuoni haonekani

Thu, 23 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Wakati sakata la tatizo la ukosefu wa maji likirejea katika maeneo ya Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) nchini Tanzania imeibuka sintofahamu ya wapi alipo mwanafunzi Mugaya Tungu.

Katika siku za hivi karibuni kuliibuka gumzo mitandaoni baada ya kusambaa kwa picha zilizowaonyesha wanafunzi wa Udom wakiwa katika foleni ndefu wakiwa na madumu ya maji.

Jana Jumatano Januari 22, 2020, Makamu Mkuu wa Udom, Profesa Faustine Bee aliomba radhi kwa jumuiya ya chuo hicho kutokana na tatizo la maji lililotokea kwa siku saba mfululizo.

Katika taarifa iliyoandikwa na Ofisi ya Mahusiano ya Umma na Masoko ya Udom ilimnukuu  Profesa Bee akisema tatizo la ukosefu wa maji katika chuo hicho lilianza Januari 12 hadi 19, 2020 ambalo lilisababishwa na kukatika kwa bomba kubwa linalopelekea maji chuoni hapo.

Hata hivyo, taarifa kwenye mitandao zinaeleza kuwa, mwanafunzi wa mwaka wa pili anayesoma sayansi asili Mugaya Tungu alikamatwa na polisi juzi Januari 21,2020 akidhaniwa kuwa ndiye aliyepiga picha hizo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwanafunzi huyo alikamatwa akiwa chumbani kwake eneo la Udom na kupelekwa kituo cha polisi cha Chimwaga lakini wanafunzi wenzake walifuatilia kituoni hapo na kumkosa huku wakielezwa kwamba mwanafunzi mwenzao huyo alishawekezwa dhamana ingawa chuoni haonekani na simu zake hazipatikani.

Pia Soma

Advertisement
Jana usiku, Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto aliliambiwa Mwananchi hana taarifa za kukamatwa kwa mwanafunzi huyo na polisi.

Katibu wa serikali ya wanafunzi wa chuo hiyo, Paschal Michael alisema hana taarifa zozote kuhusiana na mwanafunzi huyo ingawa amekiri kumfahamu.

“Mugaya Tungu namfahamu kweli, ila siyo kiongozi wa serikali ya wanafunzi lakini namfahamu, kuhusu kukamatwa na polisi sina taarifa na ndiyo nasikia kwako, ngoja nifuatilie nitakujulisha kinachoendelea,” alisema Michael.

 

mwananchi.co.tz