Fri, 8 Jul 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limesema linaendelea na uchunguzi dhidi ya mratibu wa Hamasa wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA), Twaha Mwaipaya.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma ACP Martin Otieno amesema Twaha anatuhumiwa kwa kutoa taarifa za uongo katika ukurasa wake wa Twitter kuhusu kupanda kwa gharama za umeme wakati akijua kuwa yeye sio msemaji wa shirika la umeme nchini TANESCO na kuzua taharuki kwa wananchi.
Akizungumza na wanahabari jijini humo leo Ijumaa, Julai 8, 2022, Kamanda Otieno amesema baada ya kukamilika kwa uchunguzi wanatarajia kumfikisha mahakamani wakati wowote.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live