Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yaeleza chanzo cha moto ulioua familia Mwanza

Moto Pic Data Polisi yaeleza chanzo cha moto ulioua familia Mwanza

Mon, 8 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limesema chanzo cha moto ulioua ndugu watano wa familia moja kuwa ni shoti ya umeme iliyotokea kwenye kifaa cha kuchajia simu (extension).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng'anzi amesema uchunguzi wa awali umeonyesha kwamba moto huo uliozalisha moshi mzito ulianzia sebuleni walipokuwa wamelala wageni wawili (marehemu) waliyokuwa wameitembelea familia hiyo.

Ng'anzi amewataja ndugu hao kuwa ni baba wa familia hiyo, Lameck Benedicto (32) mke wake, Leyah Lameck (26) mtoto wao, Yunith Lameck (1) na ndugu wawili waliyoitembelea familia hiyo.

"Shoti hiyo ilipotokea ilisababisha moto ambao uliashika kwenye godoro walilokuwa wamelalia wageni kisha kwenye paa hadi kusambaa kwenda chumbani huku ndugu hao wakikimbilia chumbani baada ya kushindwa kufungua mlango wa nyumba hiyo uliotengenezwa kwa chuma," alisema Ng'anzi

Kwa upande wake, Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Mwanza, Ambwene Mwakibete ametoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kutoa taarifa haraka wanapoona tukio la moto ili kurahisisha zoezi la uokoaji.

"Niwaombe wananchi wajiepushe na matumizi ya vyuma wanapojenga majengo kwa ajili ya makazi na biashara kwa sababu chuma kinaposhika moto inakuwa ngumu kukivunja ili kuingia ndani kuokoa watu na vitu," amesema Mwakibete

Chanzo: mwananchidigital