Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wazuia maadhimisho ya wanawake Chadema

45600 Pic+chadema Polisi wazuia maadhimisho ya wanawake Chadema

Sun, 10 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita. Polisi wilayani Geita limekizuia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuadhimisha siku ya wanawake duniani.

Chadema walipanga kufanya maadhimisho hayo katika ukumbi wa Moyo wa Huruma uliopo mjini Geita na kutaka wanawake wa chama hicho kuungana na wanawake wenzao katika maadhimisho ya kiserikali.

Kutokana na zuio hilo la polisi, wanawake wa vyama vya CDM na CCM wakatumia maadhimisho hayo kuvaa sare za chama na kutambiana kwa kunyoosha vidole vya ishara ya vyama vyao.

Chadema wameonekana wakiwa wamekaa katika maeneo yao wakiwa na sare zao huku kina mama wa CCM nao wakiwa na sare za chama chao katika viwanja vya soko jipya mjini Geita.

Katiba barua iliyotolewa na mkuu wa polisi wilaya, Ally Kitumbu iliyotolewa jana Alhamisi Machi 7, 2019 kwa katibu wa Chadema Geita yenye kumbukumbu namba GE/B.3/24/VOL.V11/63 imewataka wanawake kushiriki maadhimisho hayo maeneo ya Bugulula halmashauri ya wilaya na viwanja vya soko jipya yanakoadhimishwa na halmashauri ya mji.

Mbali na kuzuia maadhimisho hayo kufanywa ukumbini, pia barua hiyo imezuia matangazo yoyote yanayohusiana na kufanya maadhimisho hayo kwa itikadi za kisiasa.

Katika vipeperushi vilivyokuwa vikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii, ilionyesha Chadema Geita itaadhimisha maadhimisho hayo katika Ukumbi wa Moyo wa Huruma na mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) Halima Mdee.

Kauli mbiu ya Chadema katika maadhimisho hayo ilikuwa, “Tupambane na mfumo kandamizi nchini tupate fursa sawa za uongozi.”



Chanzo: mwananchi.co.tz