Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wawatembelea wahanga wa ajali za bodaboda

Askarti Web Polisi wawatembelea wahanga wa ajali za bodaboda

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na viongozi wa waendesha pikipiki mkoani humo, wamewatembelea wahanga wa ajali za pikipiki na vyombo vingine vya moto katika hospitali ya Nkoranga Lutheran iliyopo Arumeru kwa lengo la kutoa pole na kukusanya taarifa.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani humo SP Solomon Mwangamilo, akiongozana na askari wa kikosi hicho amesema kuwa lengo la kufika katika hospitali hiyo ni kukusanya taarifa zao na kutoa pole kwa wahanga wa ajali ambapo amebainisha kuwa hospitali hiyo ni maarufu kwa kutibu wagonjwa waliopata madhara yatokanayo na ajali mbalimbali kwa kanda hiyo.

Naye Katibu wa waendesha pikipiki wilaya ya Arusha Hakimu Msemo, amebainisha kuwa wapo baadhi ya waendesha pikipiki ambao wamekuwa wakiendesha vyombo hivyo kwa kukiuka sheria za usalama barabarani.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chama cha wendesha bodaboda wilaya ya Arusha amesema wao kama viongozi wamejifunza na kusema kuwa wanakwenda kuwa waeleza namna ajali zinavyo waacha wananchi na madhara ya kudumu.  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live