Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wavunja harusi ya msichana wa miaka 11

03396e5e1df68037f9f9d44a8f427763 Ndoa

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

JESHI la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limevunja sherehe ya harusi ya msichana mwenye umri wa miaka 11. Mtoto huyo alitarajiwa kuolewa jana kwa mahari ya ng'ombe watatu wilayani Same mkoani humo.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Simon Maigwa alisema tayari mtoto huyo alifanyiwa sherehe ya kumuaga (send off) Julai 7 mwaka huu nyumbani kwa wazazi wake kwenye Kijiji Cha Emuguri Kata ya Njoro wilayani Same.

Kamanda Maigwa alisema polisi wamemtia mbaroni baba mzazi wa mtoto huyo na kwamba jina la mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 68 na jina la aliyekuwa bibi harusi mtarajiwa yamehifadhiwa kwa sababu za kiusalama.

"Polisi ilipata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya kuwepo kwa harusi hiyo haramu nasi tukaandaa mtego ambao ulifanikisha kuvunja harusi hiyo" alisema.

Kamanda Maigwa alisema watuhumiwa wa ndoa hiyo walikamatwa Agosti 8 saa 12.00 asubuhi nyumbani kwa baba wa mtoto huyo wakiwa wanajiandaa kumpeleka binti kwa mumewe eneo la Ruvu wilayani Same.

Alisema mtoto huyo hakuwa akisoma na alionya wazazi wanaoozesha watoto wakiwa na umri mdogo na akahimiza jamii ifichue uwepo wa mipango ya ndoa haramu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz