Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi watoa kauli gari lililotumbukia baharini, dereva asalimika

Cocobeachpicfff Gari aina ya Landcruiser limetumbukia katika Bahari ya Hindi eneo la ufukwe wa Coco

Tue, 5 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Gari aina ya Toyota Landcruiser Prado limetumbukia katika Bahari ya Hindi eneo la ufukwe wa Coco huku polisi wakieleza kusubiri afya ya dereva wa gari hilo kuimarika ili waanze uchunguzi.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai ameieleza Mwananchi Digital leo Jumanne Oktoba 5,2021 kuwa hakuna madhara yoyote yaliyotokana na ajali hiyo baada ya mtu huyo kuokolewa.



Amesema wanasubiri afya yake iimarike ili wafanye uchunguzi wa tukio hilo kwa kuwa dalili zinaonyesha alikuwa ni mtu mwenye mawazo au tatizo la akili.

"Kule alipokuwa anakwenda kulikuwa hakuna barabara, kama mtu ni mzima huwezi kuona gari linakwenda baharini na wewe ukazidi kukanyaga mafuta," amesema Kingai.



Wakizungumzia tukio hilo mashuhuda wanadai tukio hilo lilitokea jana saa saba mchana baada ya kuliona gari kwenye maji na alikuwepo dereva pekee ambaye walifanikiwa kumuokoa na kumkimbiza hospitali baada kunywa maji mengi katika jitihada za kujiokoa.

Chanzo: mwananchidigital