Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi watawanya wananchi kwenye mgogoro wa ardhi Monduli

Silaa Ataka Mpango Uendelezaji Eneo La Viwanda Kibaha Polisi watawanya wananchi kwenye mgogoro wa ardhi Monduli

Sun, 17 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Arusha. Jeshi la Polisi Wilaya ya Monduli Mkoa Arusha limewatawanya wananchi wa Kijiji cha Moita wilayani humo ambao wana mgogoro wa ardhi.

Kabla ya Polisi kuingilia kati, Mkuu wa Wilaya hiyo (DC), Joshua Nassari alizungumza na wananchi hao jana Jumamosi Desemba 17, 2023 na kuwataka mgogoro huo kwa kuwa Serikali ina mpango wa kukipima kijiji hicho ili kulinda maeneo ya jamii yasiuzwe.

Katika kikao hicho, Nassari aliambana na kamati ya Ulinzi na Usalama na wananchi hao mara kadhaa walikuwa wakipinga alichokuwa anakieleza, hali iliyokuwa ikisababisha askari kuingilia kuwatuliza.

Baadhi ya wananchi kijiji hicho, walikuwa wanamtuhumu mwenyekiti wao, Bruno Joseph kwa kuuza ardhi yao kinyume cha taratibu, kwamba anadaiwa kupima viwanja 370 na kuviuza bila kujali maeneo ya huduma za kijamii na maeneo ya malisho ya mifugo.

Hata hivyo, mwenyekiti huyo alidai wanaochochea mgogoro ni wananchi wa vitongoji viwili ambavyo watu wachache wamehodhi ardhi kubwa.

“Nimekwishakukiri mbele ya ofisi na DC anajua, kwamba mimi katika utawala wangu naongoza vitongoji sita lakini kitongoji kimoja kinanipinga na kinachonipinga waliohodhi ardhi, lakini tulieni, waliohodhi wapo hawajafa,” alisema.

Nassari aliwataka wananchi kuwa watulivu akisema Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama imejipanga kumaliza migogoro katika wilaya hiyo.

"Tutakuja hapa Moita Bwawani tutapima ardhi yote ya umma na kuwa na hati moja, hivyo hakuna kiongozi ambaye ataweza kuiuza kinyume cha taratibu," alisema Nassari huku akiwataka wananchi hao kuacha siasa zisizo na ulazima.

Alisema anajua kuna watu wanakopa fedha benki kwenda kuweka rehani ardhi ya kijiji, jambo ambalo halikubaliki na yeye atasimamia ardhi hiyo ipimwe.

Hata hivyo, katika mkutano huo baadhi ya wananchi walianza kupinga mpango wa Serikali kupima tena ardhi ya kijiji ili kuweka hati moja wakisema mpango huo utaficha waliouza ardhi.

Rehema Sanare, mmoja wa wanakijiji hao alisema Serikali inapaswa kutatua migogoro ya ardhi Monduli kwani baadhi ya viongozi wa vijiji wamekuwa wakiuza ardhi kinyume cha sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live