Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi watanda Soko la Mwanjelwa, wawadhibiti wafanyabiashara

29913 Soko+pic TanzaniaWeb

Mon, 3 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Askari wameimarisha ulinzi nje ya Soko Kuu la Mwanjelwa jijini Mbeya baada ya baadhi ya wafanyabiashara kutaka kuanzisha vurugu wakipinga kuondolewa biashara zao nje ya soko hilo.

Leo asubuhi Desemba 3, 2018 wafanyabiashara ambao wamejenga vibanda ndani ya uzio wa soko hilo walionekana kutofungua vibanda vyao na kutaka kufanya fujo ambazo zimedhibitiwa na askari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amesema polisi  wamefika eneo hilo kuimarisha ulinzi ili watu waendelee na biashara zao na kuwadhibiti wenye nia ya kuvuruga mipango ya Serikali ya kuboresha ufanyaji biashara.

"Polisi wapo kwa ajili ya kuhakikisha usalama unakuwepo. Ni hao wachache tu ndiyo wanataka kuharibu tu mipango mizuri ya jiji letu. Hilo soko limejengwa kwa gharama kubwa na ni la kisasa zuri, sasa watu hawataki kuingia ndani na kutaka kufanya biashara zao nje,” amesema Matei.

“Naomba tu tuendelee kutoa elimu kwa wananchi katika hili. Tunataka wafanye biashara zao kwa uhuru lakini wale ambao wanataka kuleta vurugu tutawadhibiti, tunataka Mbeya iwe shwari.”

Juzi Jumamosi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila alifika Soko la Mwanjelwa na kutoa amri kwa wafanyabiashara hao ifikapo Ijumaa Desemba 7, 2018 wawe wamevunja vibanda vyao na kuwataka kuingia ndani ya soko hilo na watakaokaidi nguvu itatumika.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz