Dar es Salaam. Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limetoa majina ya wanafunzi watano wa shule ya msingi Ndelenyuma waliokufa baada ya kugongwa na gari jana Jumatano Februari 12, 2020 katika halmashauri ya Madaba, Songea.
Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma, Simon Maigwa amesema wanafunzi hao ni Glory Kilasi (12) alikuwa akisoma darasa la nne, Ushindi Juma (12) darasa la nne, Evaristo Miligo (10) darasa la pili, Isaya Mkani (13) darasa la nne na Victor Luoga (10) darasa la kwanza.
“Majeruhi ni Hilda Kilasa (12) mwanafunzi wa darasa la nne ambaye alitibiwa na kuruhusiwa na hali yake inaendelea kuimarika” amesema Maigwa
Maigwa amesema gari lililowagonga wanafunzi hao ni mali ya kampuni ya Camusat lililokuwa linatokea Songea kwenda Madaba liliendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina moja la Salum.
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi