Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wapiga ‘stop’ bodaboda kuingia mjini

70027 Pic+bodaboda

Mon, 5 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam nchini Tanzania limepiga marufuku bodaboda kuingia katikati ya Jiji kuanzia kesho Jumanne Agosti 6 hadi 18, 2019 utakapomalizika mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Polisi imesema zuio hilo linatokana na baadhi ya bodaboda kujihusisha na vitendo vya uhalifu.

Akizungumza na wanahabari leo Jumatatu Agosti 5, 2019, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema lengo la jeshi hilo kufimekia uamuzi wa kupiga marufuku bodaboda hizo kuingia mjini baadhi yao wamekuwa wakijihusisha na uhalifu na kutotii sheria za usalama barabarani.

“Waendesha bodaboda wamekuwa hawapendi kufuata maagizo unaweza ukamwelekeza lakini asikusikilize ni watu wa kuchepuka barabarani utakuta wakati mwingine wanaingilia kwenye misafara ya viongozi ili kuchukua hatua wasije kuingilia kwenye misafara ya viongozi wanaotarajiwa kuingia nchini kwa ajili ya mkutano wa SADC hatutaki kuwaona kuanzia kesho katikati ya jiji hili hadi hapo mkutano utakapoisha,”amesema Mambosasa.

Pia, amepiga marufuku kuweka taa za vimulimuli au za rangi rangi, taa zenye mwanga mkali (spot light) na kufunga ving’ora kwenye magari ya watu binafsi na pikipiki.

Amesema isipokuwa magari  yanayotoa huduma za dharura na kampuni binafsi ndiyo zinaruhusiwa kufunga ving’ora.

Pia Soma

Mambosasa amesema wananchi wametakiwa kuwa wavumilivu kipindi hiki cha ugeni mkubwa wa kimataifa hivyo ni marufuku kuingilia misafara ya wageni.

“Jeshi la polisi hilo limejipanga kukabiliana na kikundi chochote au mtu yeyote atakayejaribu kufanya vitendo vya uhalifu au kuvuruga amani na utulivu katika kipindi chote cha mkutano,” amesema

Pia jeshi la polisi kanda hiyo linawahakikishia usalama wageni wote waliokuja kwenye mkutano huo katika kipindi chote na wawe na uhuru kutembea mahali popote ndani ya jiji la Dar es Salaam kwani hali ni shwari.

Chanzo: mwananchi.co.tz