Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wanawake Nkasi wasaidia wazee

Wazee Pic Data3 Polisi wanawake Nkasi wasaidia wazee

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtandao wa polisi wanawake wilayani Nkasi mkoani Rukwa wametoa mahitaji mbalimbali kwa wazee baada ya kutambua mchango mkubwa kwa taifa kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kesho.

Msaada huo umekabidhiwa leo Alhamisi, Machi 7, 2024 kupitia mdahalo uliowakutanisha wananchi mbalimbali wakiwepo viongozi wa dini na machifu.

Mwenyekiti wa mtandao huo, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Ivona Mwanga amesema wao kama wanawake wanatambua mchango wa wazee katika Taifa na ndio lengo la kuwaona na kuwapatia baadhi ya vitu vya mahitaji ya nyumbani.

Mnufaika wa msaada huo, Sauda Nkana ameshukuru kwa msaada wa mahitaji muhimu kwa familia yake, kwani anaishi na wajukuu watano alioachiwa na wazazi wao baada ya kufariki kwa nyakati tofauti.

Mzee wa kimila kutoka katika kijiji cha Katuka, Deusdedit Mwananzumi amepongeza Jeshi la Polisi kwa kugusa kundi la wazee wenye mahitaji na kwamba kupitia mdahalo huo wamepata elimu.

Akizungumza baada ya kushiriki mdahalo huo, ofisa maendeleo ya jamii mkoa wa Rukwa, Anisia Ulusi amesema kila mtu kwa nafasi yake anapaswa kushirikishwa katika maamuzi kuanzia ngazi ya familia na kuondoa vikwazo ikiwepo mfumo dume kwa wanawake.

Kwa upande wake, Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjilist la Kirutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Sumbawanga ambaye ni mwenyekiti wa jumuia ya maridhiano na amani, Atupele Mwaipopo amesema wanawake wanaweza kama wataendelea kuwa wabunifu na kutumia vema rasilimali ya ardhi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live