Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi, wananchi watakiwa kujifunza kifo cha Trafiki aliyegongwa gari

Askari Kugongwa Kuagwa.png Polisi, wananchi watakiwa kujifunza kifo cha Trafiki aliyegongwa gari

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati mwili wa askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, WP. 3984 Sajenti, Stella Alfonce (49) ukitarajiwa kuzikwa Bukoba mkoani Kagera, Maofisa wa Jeshi la Polisi na wananchi wametakiwa kutumia kifo cha askari huyo kama funzo la kujiandaa na umauti.

Akizungumza leo Alhamisi Novemba 2, 2023 wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika Kanisa Katoliki Kigango cha Isegenge Kata ya Nyakato jijini Mwanza, Paroko Msaidizi wa kigango hicho, Joseph Yunga amesema kifo humtokea mwanadamu wakati wowote.

Katika misa hiyo iliyoudhuriwa na waombolezaji wakiongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Janeth Magomi, Padri huyo amewataka wanafamilia kuwa wavumilivu akidokeza kuwa hilo ni jaribu kwao kuwapima upendo wao kwa Mungu.

“Hata mimi nilikuwa nakiogopa sana kifo lakini baada ya kumwendea Mungu na kuwapoteza wapendwa wangu wakiwemo wazazi wangu ndipo nilipotambua kuwa Yesu anaishi na anaumuhimu kwenye maisha yetu. Hivyo niwaombe waombolezaji wote tumwombee mwenzetu huyu apumzike kwa amani,"amesema Padri Yunga

WP. 3984 Stella alifariki Jumatano Novemba Mosi, 2023 kwa kugongwa na gari ya shule ya Nyamuge akiwa eneo la Nyamhongolo baada ya kubaini kuwa gari hiyo inamakosa ndipo alipomwelekeza dereva, Philipo Mhina (52) kuirudisha nyuma, wakati dereva anairudisha nyuma alimgonga na kusababisha kifo chake.

Mwili wa Stella unaagwa leo kisha utasafirishwa kuelekea Bukoba mkoani Kagera kwa maziko huku mtuhumiwa akiwa rumande kwa mahojiano.

Akizungumza kwa niaba ya familia shemeji wa marehemu, Francis Mganyizi amesema familia inachukulia tukio hilo kama funzo la kujitoa kwa taifa ambapo amesema wanaamini mpedwa wao amefariki akilitumikia Taifa.

"Tunashukuru Jeshi la Polisi kwa kutambua uzalendo ambao Stella ameuonyesha kwa Taifa lake. Hatuna wa kumtupia lawama badala yake tunamwachia Mungu,”amesema Mganyizi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live