Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wamkamata ‘baba’ akiwa uchi na mtoto

89425 Baba+pic Polisi wamkamata ‘baba’ akiwa uchi na mtoto

Fri, 20 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Mtu mmoja ambaye jina lake halijafahamika anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Morogoro baada ya kukutwa mtoni na mtoto mwenye umri kati ya miaka mitano hadi 10, wote wakiwa hawana nguo huku akiwa na panga na msumeno.

Tukio hilo limetokea jana Alhamisi Desemba 19, 2019 katika maporomoko ya maji ya Nguzo Camp mkoani humo, video zake kuanza kusambaa leo asubuhi katika mitandao mbalimbali ya kijamii, zikimuonyesha akiwa na mtoto kwenye maji na watu wakifanya jitihada za kuwaokoa.

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa  kuzungumzia tukio hilo, amesema atalitolea maelezo ya kina kesho Jumamosi Desemba 21, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari.

Taarifa ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa wakati mtu huyo akiwa katika maporomoko ya maji kwenye mto huo, askari waliokuwa katika shughuli nyingine walimuona na kumtilia shaka

“Walipomuona alijitosa kwenye maji ya kina kirefu akiwa na  mtoto aliyekuwa akipiga kelele akisema ‘baba unaniua, baba unaniua’,” zinaeleza taarifa hizo.

“Walifanikiwa kumtoa katika maji akiwa na mtoto huyo na anashikiliwa na polisi. Mtoto naye yupo salama.”

Chanzo: mwananchi.co.tz