Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wakamata gari iliyokuwa ikitumika kuwaibia wananchi

Polisi Wakamata Gari Iliyokuwa Ikitumika Kuwaibia Wananchi Polisi wakamata gari iliyokuwa ikitumika kuwaibia wananchi

Tue, 15 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoa Tanga  limefanikiwa kukamata gari aina ya Toyota  Ractis yenye No.T.515DXR iliyokuwa ikitumika Kuwaibia watu mbalimbali ,huku likikamta pikipiki 18 zilizokamatwa kwa makosa mbalimbali ya Jinai.

Akitoa taarifa ya kipindi cha mwezi Oktoba  mwaka huu ya misako ya Operesheni iliyofanyika ya mapambano dhidi ya  uhalifu na wahalifu mkoani Tanga, Kamishna  msaidizi mwandamizi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Tanga Henry Mwaibambe  alisema jeshi hilo linaendelea kupambana na uhalifu  na wahalifu wanaojihusisha na makosa mbalimbali uliofanyika kwa nystatin tofauti.

Aidha ailisema kuwa mnamo tarehe13 October mwaka huu majira ya saa 11:30 huko maeneo ya Bank ya CRDB  iliyopo kata ya cental Tarafa ya Ngamiani Kaskazini  jijini Tanga ,ilikamatwa gari NO.T.515 aina ya Toyata Ractis ilikamatwa na mtuhumiwa alikimbia ambapo mtuhumiwa hutumia maeneo kuwaibia watu mbalimbali  kwa utapeli.

Kamanda Mwaibambe  alisema kuwa wakati mwingine mtuhumiwa huyo  huiba kutoka ndani ya Magari  ya wananchi wanaofuata huduma katika banki hiyo,hivyo jeshi la polisi linaendelea kumtafuta ili afikishwe  kwenye mikono ya sheria.

Katika hatua nyingine  kamanda mwaibambe alisema kuwa wamefanikiwa kakamat pikipiki 18 katika misako hiyo ya operesheni ya ndani ya mwezi moja ambapo zilikamatwa kwa makosa mbalimbali ya jinai.

Aidha Mwaibambe  alitaja idadi ya pikipiki hizo katika misako inauoendelea kuwani 18 ambapo kati ya hizo pipiki 3zilikamatawa kuhusiana na uwizi wa mifugo pamoja watuhumiwa 3 wilayani Muhe,a mkoani Tanga. Aid

Sambamba hayo alisema pipiki  12 zilimakamatwa kwa makosa ya unyang'anyi wa kutumia nguvu na uporaji  wa simu haswa mikoba ya kinamama ambapo watuhumiwa saba wamekatwa watafikishwa mahakamani kuhusiana na tukio hilo.

Hata alisema pikipiki 3 zilikamatwa kuhusiana na makosa ya usafirishaji wa Dawa za kulevya  pamoja na usafirishwaji wahamiaji haramu ambao  wameingia nchini bila Kibali.

Katika tukio nyingine alisema jeshi la polisi limefanikiwa kamata silaha bandia katika mkoa wa Tanga  ambapo mnamo tarehe 3 October mwaka huu majira ya saa saba mchana huko katika maeneo ya kisosora kata ya Nguvumali tarafa ya Chumbageni katika jiji la Tanga alikamatwa Huruma John akiwa na silaha( Pistal)bandia  oliyokuwa kwenye bagi lake la mgongoni  ambapo mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live