Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wakamata bajaji 57, madereva 10 Morogoro

74398 Bajaj+pic

Thu, 5 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Polisi mkoani Morogoro wamekamata bajaji 57 na madereva 10 baada ya madereva wake kuzitelekeza wakati wa operesheni ya kuwaondoa katika eneo la Boma Road.

Hatua hiyo imesababisha barabara kufungwa kwa muda manispaa ya Morogoro leo Alhamisi Septemba 5,2019.

Bajaji hizo zinazofanya kazi ya kusafirisha abiria ndani ya manispaa hiyo, zilikamatwa na askari mgambo baada ya kuegeshwa katika lango kuu la kuingia stendi kuu ya daladala zinazoenda nje ya manispaa ya Morogoro zikipakia abiria na kushusha.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema jeshi hilo likishirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama wamekamatwa bajaji 57 na madereva 10.

Amesema leo saa 12 asubuhi askari mgambo wa Manispaa ya Morogoro wakiwa katika kazi maalumu ya kuondoa bajaji barabara za Boma Road, Madaraka na Mahenge, madereva wake walizitelekeza barabarani na kusababisha barabara hizo kufungwa kwa muda dakika 22 kabla ya kufungua.

“Barabara ya Korogwe na Madaraka ilifunguliwa saa 9:20 asubuhi baada ya kufungwa saa 8:58 asubuhi baada ya bajaji hizo kutelekezwa barabarani na madereva wake katika barabara za Madaraka na Korogwe,” amesema Mutafungwa.

Pia Soma

Advertisement
Kamanda Mutafungwa amesema bajaji hizo baada ya kukamatwa zilihifadhiwa kituo kikuu cha polisi na baadaye kuhamishiwa yadi ya Manispaa ya Morogoro ambapo madereva 10 walikamatwa na wengine kutoroka na askari wanachukua jukumu la kuwasaka na itawachukulia hatua za kisheria.

Dereva wa bajaj kituo cha Islam, Hussein Omari amesema vituo wanavyopangiwa na mamlaka husika sio rafiki kwao katika kufanya biashara ya kubeba abiria huku akieleza madai yao kusababisha msongomano sio kweli.

Kwa dereva mwingine, Ismail Halfan amesema kuondolewa kwao maeneo hawakushirikishwa lakini huo ndio mwanzo kwao wa kukutana na viongozi wa Manispaa, Wakala wa barabara vijijini na mijini (Tarura) na jeshi la polisi upande wa usalama barabarani na kusikiliza changamoto zao.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz