Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi waitaka familia iliyosusa mwili mochwari kwenda kuuchukua

13301 Muhimbili+pic TanzaniaWeb

Thu, 23 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Polisi Mkoa wa Temeke leo Jumatano Agosti 22, 2018 wameitaka familia iliyosusia mwili wa ndugu yao uliopo mochwari kwenda kuuchukua kwa ajili ya maziko.

Salum Kindamba aliuawa hivi karibuni eneo la Jet Lumo ikidaiwa ni kwa kupigwa risasi na polisi na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) tangu mwanzoni mwa wiki iliyopita.

Familia ya marehemu imetaka Serikali iunde tume kuchunguza mazingira ya kifo chake, vinginevyo wataendelea kuuacha mwili mochwari.

Akizungumza leo Agosti 22, Kamanda wa polisi Temeke, Emmanuel Lukula amesema uchunguzi wa tukio hilo umefanyika tangu Agosti 13, 2018, ripoti kukabidhiwa kwa ndugu, kwamba wanapaswa kwenda kuchukua mwili kwa ajili ya maziko.

Amesema upelelezi uliofanywa umebaini kuwa marehemu alikuwa akijihusisha na vitendo vya uhalifu na ndio sababu alikimbia baada ya kuwaona polisi.

Akizungumzia mazingira ya kujeruhiwa kwa marehemu amesema Agosti 11, 2018 walipokea taarifa eneo la Kiwalani Kigilagila kuna watu wanne wenye mfuko wenye silaha.

“Polisi walifika eneo la tukio ili kuwabaini watu hao na walipotaka kufanya nao mahojiano mmoja kati yao (Kindamba) alikimbia akiwa na mfuko huo,” amesema.

Soma Zaidi:

...Muhimbili yafanunua kilichomuua Salum Kindamba

Amesema polisi walifyatua risasi hewani ili asimame lakini alikaidi na katika juhudi za kumkamata risasi ilimjeruhi mguuni na mkononi.

“Polisi walifanya kila jitihada za kufanikisha kumkamata mtuhumiwa lakini alikaidi, kutokana na jeraha alilopata tulimkimbiza hospitali ya Temeke na baadae alifariki dunia,” amesema.

Amebainisha kuwa kati ya  watuhumiwa wanne watatu walijisalimisha kwa polisi ambao ni Moses Halamela (30), Agape Mwakanyamale (34) na Omari Mhando (33).

Kuhusu mwili wa marehemu kutochukuliwa, amesema Lukula amesema  wanachotaka ni kupewa ripoti ya uchunguzi ambayo kwa hatua za awali ripoti hiyo ni mali ya daktari na jeshi la Polisi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz