Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi waingia kitaa kuzibua mitaro maji machafu

Mitaro Polisi Usafi Polisi waingia kitaa kuzibua mitaro maji machafu

Fri, 13 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limeingia mtaani kufanya usafi na kuhimiza wananchi kushiri katika kuweka mazingira safi ili kudhibiti magonjwa ya mlipuko.

Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha na Mrakibu mwandamizi wa Polisi SSP George Malema amesemawakati wakifanya usafi katika soko la kilombero lililopo halmashauri ya Jiji la Arusha kuwa dhamira ya Jeshi hilo ni kuhimiza usafi ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.

Malema amesema kuwa Jeshi hilo linadhamana ya kuwalinda wananchi pamoja na mali zao ambapo amebainisha kuwa wao wanaona fahari kuwahudumia wananchi wanaoishi mazingira safi na salama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live