Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi waendelea na uchunguzi watoto waliokufa maji Mtwara

34710 Wafa+maji+pic Tanzania Web Photo

Fri, 4 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtwara. Jeshi la Polisi mkoani Mtwara limesema bado linachunguza vifo vya wanafunzi wawili wa Shule ya Msingi Mgao wanaodaiwa kufa maji katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, eneo la Mgao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Januari 3, 2019, Kamanda wa jeshi hilo mkoani humo, Blasius Chattanda amesema tukio hilo limetokea Januari Mosi, 2019.

Chattanda amewataja wanafunzi hao kuwa ni Rajab Athuman (12) aliyekuwa akisoma darasa la nne na Salum Maleka (8) aliyekuwa darasa la kwanza.

“Tunaendelea na uchunguzi kubaini kama watoto hao wamezama kwa uzembe ama ni ajali ya kawaida kwani tahadhari ilitolewa kwa wananchi wote kutowaacha watoto kwenda peke yao ufukweni hasa kipindi cha sikukuu,” amesema Chattanda.

Wakati huohuo, amesema polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini watu waliomshambulia Amri Nayope (16) na kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Newala.

“Baada ya kushambuliwa maeneo mbalimbali ya mwili na watu wasiofahamika walimtelekeza karibu na nyumba yao. Waliofanya tukio hilo lazima wakamatwe na polisi maana kujichukulia sheria mkononi si jambo sahihi,”amesema.



Chanzo: mwananchi.co.tz