Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wachunguza mwanaume aliyenajisi watatu wa familia moja

373ffc516c4f63abe1f41c9a94a379f6.PNG Polisi wachunguza mwanaume aliyenajisi watatu wa familia moja

Sun, 27 Mar 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Jeshi la Polisi mkoani Geita linamchunguza mwanaume mmoja (jina linahifadhiwa) mkazi wa Kata ya Bukori wilayani Geita kwa tuhuma za kuwaingilia kimwili watoto watatu wa familia moja.

Mwanaume huyo ambaye bado hajakamatwa alikuwa anaishi familia moja na watoto hao na anadaiwa kufanya ukatili huo wa kingono kwa muda mrefu pasipo kujulikana na kupelekea athari kubwa ya kimwili kwa watoto hao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe alithibitisha na kutoa taarifa hiyo juzi wakati akifunga mafunzo ya siku tatu ya kupinga ukatili kwa waendesha bodaboda mjini Geita.

Alifafanua kuwa watoto waliofanyiwa ukatili huo wote ni jinsia ya kike na wanasoma shule ya msingi (jina linahifadhiwa) mmoja akiwa darasa la tatu, mwingine darasa la nne na mwingine darasa la tano. “Tumepata hizi taarifa baada ya huyu mtoto mmoja kuanguka chooni (shuleni) wakati akijisaidia ndio akagunduliwa na kupelekwa hospitali na walimu ndio tukagundua haya.

Ni rai yangu kwa jamii, kama mama zetu wanajua, kwa utamaduni wetu mama unapaswa kumkagua mtoto wa kike, unamkagua makuzi yake, sasa tumekuwa kwenye biashara nyingi, vikoba, hatuangalii maendeleo ya mtoto.

“Jamii nyingi za Kiafrika, huwa watoto wanakaguliwa, ndiyo mila za kawaida, sasa msiwaache watoto waingie darasa la tano, la tatu la nne, kwa sababu mtoto anaweza kuoga mwenyewe, anafua nguo mwenyewe, anapiga pasi mwenyewe basi amekua, hapana,” alishauri.

Kamanda Henry Mwaibambe alikiri kuwa hadi sasa kuna tatizo kubwa la ukatili wa watoto unaotokea ngazi ya familia na imekuwa ngumu kufichuka kutokana na wanafamilia wengi kutokuwa tayari kutoa taarifa na ushahidi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz