Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi kuchunguza Askari Doria aliemshambulia Mwananchi

Kamanda Wa Polisi Mkoa, Alex Mkama Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limesema linafuatilia malalamiko ya Wolter Fuime (32), Mkazi wa Mjimwema ambaye analalamika kushambuliwa na Askari Polisi waliokuwa doria

Kamanda wa Polisi Mkoa, Alex Mkama-SACP amesema mnamo Mei 26, 2024 Askari Polisi walifika kwenye banda la Wolter analotumia kuonesha video, akieleza walienda kufanyia kazi taarifa fiche zilizodai eneo hilo linatumiwa kufanya matendo yaliyo kinyume na maadili ikiwemo kuonesha picha za video zisizo na maadili kwa Watoto, ambapo walimkamata Walter na baadaye kumwachia kwa dhamana

Mkama amesema “Baadaye Mtuhumiwa alilalamika kutojisikia vizuri, hivyo akaomba hati ya kutibiwa, akapewa. Kwa kuwa kila hati ya matibabu inayotolewa lazima kuwe na uchunguzi, hivyo tumechukua hatua ya kulichunguza suala hilo kubaini ukweli.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live