Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi haina taarifa za tukio la mwanafunzi kujirusha ghorofani

Udom Jy.jpeg Polisi haina taarifa za tukio la mwanafunzi kujirusha ghorofani

Mon, 19 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limesema halina kesi yoyote inayohusiana na mwanafunzi aliyejirusha kutoka ghorofani kwenye majengo ya Chuo Kikuu cha Ddodoma (Udom).

Desemba 14, ililiripotiwq taarifa ya mwanafunzi wa chuo hicho, Ezekiel Sostenes anayesoma ndaki ya Afya kujirusha kutoka ghorofani hadi chini kwa kinachodaiwa alitaka kujiua.

Tukio hilo lilielezwa kutokea Desemba 13 chuoni hapo, kwa kile kilichoelezwa kuwa mwanafunzi huyo alikuwa akimlalamikia mkufunzi wake kumfelisha masomo yake makusudi.

Hali hiyo ilisababisha kijana huyo kupata maumivu kiunoni na uti wa mgongo hata akalazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya rufaa ya Benjamin Mkapa.

Kosa alilolifanya la kutishia kujiua linatafsiriwa kama kosa la jinai ambalo mhusika alipaswa kuwa na kibali cha Polisi (PF3) ili aweze kupatiwa matibabu.

Akizungumzia tukio hilo leo Jumatatu Desemba 19, 2022, Kamanda wa Polisi Mkoa, Martin Otieno amesema hakuna jalada lililofinguliwa kuhusiana na tukio hilo.

"Taarifa hizo ninazo lakini kupitia vyombo vya habari, kwetu sisi ni unreported (haijaripotiwa) kwa hiyo ni ngumu kueleza kuna nini kinaendelea," amesema Otieno.

Majibu ya Kamanda yanazidi kuongeza maswali kwa tukio hilo ambalo limekuwa na sintofahamu kwa chuo na mhusika.

Upande mmoja, unasema Ezekiel alijirusha huku akiacha ujumbe kuwa anafanya hivyo kutokana na kuchoshwa na suala la kurudia mitihani kwamba amekuwa akifelishwa.

Hata hivyo uongozi wa chuo ulitoka hadharani kupinga kauli hiyo wakisema kilichotokea ni hasira za kuachwa na mpenzi wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live