Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi chanzo cha msongamano bodaboda vituoni

Piki Na Polisi.jfif madereva boda boda na Polisi

Thu, 12 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya madereva wa magari na bodaboda manispaa ya Morogoro wamesema moja ya sababu ya kutelekezwa kwa vyombo vya usafiri kwenye vituo vya polisi ni kurundikiwa makosa na kutozwa faini.

Akizungumza na mwanahabari mmoja wa madereva wa bodaboda, Osward Nyamoga amesema askari wa usalama barabarani wamekuwa wakitoza faini kubwa zinazolenga kuwakomoa hivyo wanashindwa kuzilipa hiyondo sababu moja kubwa inayopelekea wao kuacha boda zao polisi, aliongeza kwa kulalamika kesi inapofika kutuo cha polisi baada ya kukamatwa mapolisi wanakuwa na mlolongo mrefu.

"pikipiki inapokamatwa kwa ajili ya uchunguzi na kukuta makosa madogo wakisema twende kituoni mlolongo unanzia hapo mara wadai risiti ulizonunulia na hapo ndio mwanzo wa njoo kesho, njoo keshokutwa mpaka siku zinaenda mtu anaamua kuitelekeza na kufanya mambo yake mengine maana tayari biashara yetu inakuwa imekwama. "

Hata hivyo dereva mmoja wa teksi Shabani Musa ambaye anayeegesha eneo la Tanesco alijitokeza nakusema kuwa vyombo hivyo vinakaa muda mrefu kwenye vituo vya polisi na matokeo yake baadhi ya vifaa kama 'site miller', vitasa vya milango na taa vinachomolewa."Na sio vifaa tu hata mafuta wananyonya na siku ukienda kuchukua gari hakuna wa kumdai wala kumlalamikia," alisema Musa.

kaimu mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Morogoro Ahimidiwe Msangi amesema, tatizo la madereva ama wamiliki wa vyombo vya usafiri kutelekeza vyombo vyao mkoani Morogoro sio kubwa kama miaka ya nyuma,kufuatia kupungua kwa faini kutoka 30,000 hadi 10,000 kwa kosa moja madereva wameonekana wakimudu gharama hzio na hivyo kuchukua vyombo vyao mapema.

Amesema kuwa sehemu kubwa ya bodaboda na magari yaliyopo kwenye vituo vya polisi yale yaliyosababisha ajali na kesi zipo mahakamani.

Kuhusu Polisi kupiga mnada vyombo vya usafiri vilivyotelekezwa kwa kushindwa kulipa faini Msangi amesema utaratibu uliopo kabla ya kupigwa mnada ni kutoa matangazo kwenye magazeti na baadaye kupeleka taarifa hiyo makao makuu ya Polisi na kwenye mamlaka nyingine kama TRA na LATRA.

"Vyombo vya usafiri vikitelekezwa hapa kwetu kwa zaidi ya miezi sita bila mmiliki kujitokeza sisi tunahesabu hicho chombo hakina mwenyewe tunalazimika kukipiga mnada kwa kufuata sheria na taratibu zote," amesema Msangi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live