Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi: Wanasiasa saidieni kukomesha kamchape Kigoma

Wanasiasa Zitto Kamchape (600 X 317) Polisi: Wanasiasa saidieni kukomesha kamchape Kigoma

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma limewaomba viongozi wa kisiasa, kijamii na wote wenye ushawishi kwa umma mkoani humo kusaidia vita dhidi ya vitendo vya waganga wa kienyeji maarufu kama lambalamba au kamchape wanaozunguka kwenye nyumba za watu wakidai kutoa uchawi.

Akizungumza na Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe aliyefika Kijiji cha Kazuramimba Wilaya ya Uvinza katika muendelezo wa ziara ya kichama mkoani Kigoma, Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) Wilaya ya Uvinza, Alfred Mwalubilo emesema vitendo vya kamchape vina madhara ya kijamii na kiusalama.

"Sisi Jeshi la Polisi tunatumia mamlaka ya kisheria kudhibiti vitendo vya kamchape kutokana na matukio ya vurugu vinavyohatarisha amani na usalama; lakini ni rai yetu kwamba viongozi wa kisiasa, kijamii na watu wenye ushawahi kwa jamii mkoani Kigoma wanaweza kusaidia kukomesha vitendo hivi ambavyo tayari vimesababisha madhara ikiwemo vifo, majeruhi na uharibifu wa mali," amesema Mwalubilo.

Kiongozi huyo wa Polisi wilaya ametoa mfano wa vurugu vinavyohusishwa na kamchape vilivyotokea Oktoba 4, 2023 na kusababisha vifo vya watu watatu huku wengine kadhaa wakiwemo askari polisi wawili wakijeruhiwa kuwa mfano wa madhara ya vitendo hivyo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Philemon Makungu, watu 49 walishikiliwa kwa mahojiano kuhusiana na virugu hizo zilizoibuka kati ya wanaunga mkono na wanaopinga shughuli za kamchape au lambalamba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live