Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Tanzania yapiga marufuku ufyatuaji fataki

90430 Mambosasa+pic Polisi Tanzania yapiga marufuku ufyatuaji fataki

Tue, 31 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam nchini Tanzania, Lazaro Mambosasa amepiga marufuku wananchi kufyatua fataki bila kibali kutoka kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Desemba 31, 2019, Mambosasa amesema jeshi hilo halitasita kumchukuliwa hatua za kinidhamu mwananchi yoyote atakayekiuka taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.

“Wasiokuwa na kubali hawataruhusiwa kufyatua fataki na aliyepata kibali hicho ruksa kufyatua na tutamlinda lakini pia kuna mipaka yake, fataki ambazo zitakuwa na sauti kama mabomu ambayo yataleta taharuki hayataruhusiwa,” amesema.

Amesema jeshi hilo limejipanga kuimarisha ulinzi katika maeneo yote.

Amesema hali ya usalama kwa kipindi chote cha mwaka 2019, imeendelea kuimarika na kubainisha matukio makubwa ya kutumia silaha yamepungua.

“Hii imetokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa na zilizofanywa na jeshi hili ni kupikana na jitihada mbalimbali tulizofanya kwa kushirikiana na vyombo vingine vya na usalama na wananchi kuendelea kupata taarifa za uhalifu katika kipindi chote cha mwaka 2019,” amesema.

Katika hatua nyingine, jeshi hilo limewataka wananchi kufanya ibada ya mkesha wa mwaka mpya leo Jumatano usiku kwa amani na kutahadharisha kuweka maeneo yao katika hali za usalama kabla hawajaenda kwenye ibada hiyo.

“Nawafahamisha kwamba jeshi la polisi tumeimarisha ulinzi maeneo yote ya ibada ambazo zinakuwa na mikesha kuelekea mwaka mpya ikiwamo uwanja wa taifa na makanisa mbalimbali ambayo yametoa taarifa,” amesema.

“Lengo ni kuhakikisha waumini wanafanya ibada hiyo wanakuwa salama. Lakini pia nitoe rai kwa wazazi, washerehekee sikukuu hii na familia zao, kuna baadhi ya wazazi wanaacha watoto wanazurura peke yao hii ni hatari,” amesema

Chanzo: mwananchi.co.tz