Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Tabora wamdaka mtuhumiwa anayeuza dawa zilizoisha mda wake

26967 Pic+dawa TanzaniaWeb

Tue, 13 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Polisi mkoa wa Tabora linamshikilia Rajab Ramadhan mkazi wa Kazima mkoani humo kwa tuhuma za kuuza dawa za binadamu zilizoisha muda wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema mkazi huyo amekamatwa jana Jumatatu Novemba 12, 2018 maeneo ya darajani, kata ya Ipuli, manispaa ya Tabora.

Mtuhumiwa huyo alikiwa akiuza dawa mbalimbali ambazo haziruhusiwi kuuzwa mitaani huku zikiwa na nembo ya Bohari ya Kuu ya Dawa (MSD).

Kamanda Nley amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.



Chanzo: mwananchi.co.tz