Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Ruvuma wajiweka tayari

Polisi Ruvumaaa Polisi Ruvuma wajiweka tayari

Mon, 10 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu wa Jeshi la Polisi CP Suzan Kaganda amefunga mafunzo ya utayari kwa askari wa Jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma ambapo amewataka kutumia vizuri mafunzo hayo katika kufanya kazi lakini pia kuwajengea utayari ikiwa nchi inaelekea katika uchaguzi

"Mafunzo haya yalilenga kuwajengea uwezo najua miongoni mwenu wapo walioona mwanzo haya mafunzo ni ya nini lakini nyinyi wenyewe ni mashuhuda kuna mabadiliko muwajengee uwezo sio tu wa vitendo vya kijeshi lakini uwezo kwa maana ya nini mnatakiwa kama wakaguzi kati kwenye jamii lakini kama wakaguzi wa jeshi la polisi katika kutekeleza majukumu yetu ya kiutendaji wote mnaelewa tunaelekea kwenye uchaguzi kwa hiyo ni vyema kujipanga sasa na kuhakikisha kwamba mna utayari wa nini ambacho mtaenda kukifanya tunapoenda mbele kusimamia majukumu yetu kama askari.Amesema CP Kaganda.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma limezindua bwalo la polisi ambalo litasidia kuongeza faida na kusogeza huduma kwa askari wanao ishi kambini pamoja na wananchi wanao zunguka jirani ikiwa ni kuileta jamii karibu na polisi.

Lengo kuu ya kujenga kantini hii ilikuwa ni kuongeza faida na kusogeza huduma kwa askari wanao ishi kambini pamoja na wananchi wanao zunguka maeneo jirani aidha ilikuwa ni kuileta jamii karibu kabisa na jeshi la polisi na kuboresha maeneo ya burudani ya askari na kuwa sehemu tulivu kabisa na salama kwa askari na wananchi baada ya kazi ngumu za kujenga taifa.Amesema ACP Marco Chilya kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live