Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Mwanza yafanya msako wa wahalifu

Mbaroni Polisi Mwanza yafanya msako wa wahalifu

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza Wilbrod Mutafungwa amesema kuwa kuanzia sasa Jeshi la Polisi limeanza kuendesha oparesheni kali kwa wale wote wanaojihusisha na vitendo vyote vya uhalifu ikiwemo uporaji na utapeli.

Hatua hiyo imekuja kufuatia kukithiri kwa malalamiko kutoka kwa wakazi wa kata ya Buhongwa jijini Mwanza wakidai kuwepo na watu wanahojihusisha na vitendo vya uporaji na utapeli.

Kamanda Mutafungwa ametangaza opareshi hiyo wakati wa mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero mbalimbali za kiusalama kwa wakazi wa kata ya Buhongwa na Lwanhima ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kutembelea kata zote ndani ya Mkoa wa Mwanza kwa lengo la kusikiliza kero za kiusalama na kutoa elimu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live