Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Mkoa wa Kilimanjaro waonya wamiliki kumbi za starehe

89752 Knjaro+pic Polisi Mkoa wa Kilimanjaro waonya wamiliki kumbi za starehe

Tue, 24 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro limewataka wamiliki wa kumbi zote za starehe kuhakikisha zinaingiza watu kulingana na uwezo wake katika kipindi chote cha sikukuu  za mwisho wa mwaka.

Pia, limesema wakishindwa kufanya hivyo, watawajibika kisheria.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Desemba 23, 2019 na Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Salum Hamduni alipozungumza na Mwananchi katika mahojiano maalumu jinsi lilivyojipanga kuimarisha ulinzi na usalama katika kipindi chote cha sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya.

Amesema. “Rai yangu kwa wamiliki wa kumbi za starehe Mkoa wa Kilimanjaro katika kipindi hiki, wote wahakikishe wana accommodate watu kulingana na uwezo wa kumbi zao na wakishindwa kufanya hivyo watawajibika kisheria ,” amesema Kamanda Hamduni.

Kamanda huyo, amewataka pia wamiliki hao kuhakikisha wanaweka mifumo ya ulinzi ili kuhakikisha usalama wa mali za wateja wao kwa sababu kunakuwa na mkusanyiko wa makundi tofauti. “Lakini sisi kama jeshi la polisi, tutaimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yote.”

Chanzo: mwananchi.co.tz