Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Mbeya yaonya mtoto aliyetoweka

43650 Pic+mtoto Polisi Mbeya yaonya mtoto aliyetoweka

Tue, 26 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limesema linachunguza tukio la kupotea kwa mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Lyoto.

Mwanafunzi huyo, Aida Chaula (17) (pichani), alitoweka nyumbani kwao tangu Februari 11, ikiwa ni mwendelezo wa watoto kupotea sehemu mbalimbali nchini.

Kamanda wa polisi wa Mbeya, Ulrich Matei alitoa kauli hiyo baada ya kuhojiwa na Mwananchi jana kuhusu tukio hilo ambalo liliripotiwa na familia ya mwanafunzi huyo katika kituo kidogo cha polisi cha Ilomba jijini hapa.

“Tukio hilo sina taarifa nalo, lakini nitamwagiza OCD kulifanyia uchunguzi kuanzia sasa,” alisema Kamanda Matei.

“Endapo itabainika kuna mtu amemrubuni na anaishi naye kinyumba, hatua kali zitachukuliwa kwa sababu ni kosa la jinai na kumnyima haki yake ya kupata elimu mtoto huyo wa kike.”

Alisema kumekuwa na kasumba kwa baadhi ya wanaume kuwarubuni wanafunzi wa kike, jambo ambalo linakatisha ndoto zao za kupata elimu na kusababisha kuishi maisha duni na kupata mimba za utotoni.

Akizungumza na Mwananchi nyumbani kwake jana, kaka wa mwanafunzi huyo, Essau Chaula alisema mdogo wake alitoka nyumbani Februari 11 kwenda shuleni, lakini tangu siku hiyo hawajamuona.

Chaula alisema wamefanya kila jitihada za kumtafuta maeneo mbalimbali bila mafanikio licha ya kutoa taarifa polisi.

“Kimsingi tuko njiapanda, hatujui kama yuko hai au la na mimi ndiye nilikuwa nikiishi naye zaidi ya miaka sita sasa,” alisema.

“Tunaomba msaada mkubwa kwa Jeshi la Polisi ili kufanikisha kupatikana.”



Chanzo: mwananchi.co.tz