Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi: Mauaji yapungua asilimia 34 Geita

Jongo Ed Polisi: Mauaji yapungua asilimia 34 Geita

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amesema kuimarika kwa hali ya ulinzi na usalama mkoani hapa imesaidia kupunguza takwimu za matuko ya mauaji ya kikatili kwa zaidi ya asilimia 34.

Kamanda Jongo amesema hayo mjini Geita mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Ongea Nao’ inayolenga kuzuia, kutanzua na kupambana na uharifu kwa kutumia jamii.

Amebainisha kuwa takwimu zinaonesha kwa kipindi cha Januari hadi Oktoba 2022 yaliripotiwa matuko ya mauaji 49 lakini kwa Januari hadi Oktoba 2023 yameripotiwa matukio ya mauaji 32 pekee.

“Lakini matukio ya kubaka mwaka jana (2022) yalikuwa 86 na mwaka huu (2023) tuna matukio 75, huku matukio ya kulawiti mwaka jana yalikuwa saba na mwaka huu ni matukio sita.

“Lakini matukio ya shambulio la kudhuru mwili, mwaka jana tulikuwa na matukio 26 na mwaka huu tuna matukio 21, lakini matukio ya mimba za mashuleni mwaka jana zilikuwa 27 na mwaka huu tuna 25.

“Pia mwaka jana kulikuwa na matukio 39 ya kutekeleza familia lakini mwaka huu tuna matukio 20 tu, kwa hiyo kwa takwimu hizi chache mnaona namna gani hizi kampeni zinaenda zikipunguza uharifu.” -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live