Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi: Marufuku vigodoro, disko toto Dar

32919 Vigolopic Tanzania Web Photo

Sat, 22 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku vigodoro na disko toto katika sikukuu ya Krisimasi kwa kuwa vitendo vinavyofanyika katika shughuli hizo ni kinyume na utamaduni wa Watanzania.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Desemba 22, 2018 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.

Mambosasa ametoa kauli hiyo wakati akieleza jinsi polisi walivyojipanga kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka, huku akitahadharisha vitendo vya uvunjifu wa amani akiwataka wananchi kusherehekea kwa amani na utulivu.

"Doria zitaimarishwa kwenye maeneo yote zikiwemo nyumba za ibada, fukwe,  sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu," amesema Mambosasa.

“Katika sikukuu hizo polisi haitaruhusu disko toto na ngoma za vigodoro kwa kuwa zinakwenda kinyume na utamaduni wa nchi.”

Ameongeza, "Disko toto ni marufuku Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Watu washerekee na watoto wao kwenye maeneo ambayo ni salama ili sikukuu hii isije ikatuletea misiba isiyo ya lazima.”

Amewataka wazazi kuhakikisha watoto wanakuwa katika mazingira salama, kuhakikisha hawatembei wenyewe.

"Watu wanywe kwa kiasi kwa sababu maisha yapo hata baada ya Krismasi, maisha yapo hata baada ya Mwaka mpya," amesisitiza Mambosasa.



Chanzo: mwananchi.co.tz