Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Mara yakamata wanane kwa wizi wa vifaa vya ujenzi

Polisipicc Polisi Mara yakamata wanane kwa wizi wa vifaa vya ujenzi

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: mwananchidigital

Watu wanane wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Bunda Mkoa wa Mara kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa vifaa vya ujenzi kwenye mradi wa ujenzi wa barabara ya Bulamba-Nyamuswa wilayani humo.

Akitoa taarifa kwa waziri wa ujenzi aliyetembela mradi huo leo Ijumaa Desemba 17, 2021, Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Joshua Nassari amesema kuwa watu hao watafikishwa mahakamani muda wowote.

Amesema kuwa mbali na kukamatwa kwa watu hao lakini pia wanawatafuta watu kadhaa wanaodaiwa kuwa nyuma ya mtandao huo wa wizi ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Amesema kuwa vitendo vya wizi wa vifaa vya ujenzi kwenye mradi huo wenye urefu wa kilomita 46 vilikithiri sana kwa kipindi cha nyuma hali iliyopelekea uongozi wa serikali wilayani humo kuagiza kubadilishwa kwa kampuni ya ulinzi iliyokuwepo.

Awali akizungumzia uhalifu huo, Mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi ya Stasco inayolinda mradi huo, Samweli Magita amesema kuwa watu hao wamekamatwa Desemba 15, 2021.

Amesema kuwa watu hao wanatuhumiwa kuiba vifaa vya ujenzi kama vile petroli lita 70 sambamba na mifuko kadhaa ya saruji na vitu vingine vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh179 milioni huku mtu mmoja akitafutwa.

Chanzo: mwananchidigital