Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Manyara waeleza walivyojipanga kisayansi sikukuu ya Krisimasi

89836 Manyara+pic Polisi Manyara waeleza walivyojipanga kisayansi sikukuu ya Krisimasi

Thu, 26 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Babati. Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara nchini Tanzania, Paul Kasabago amesema askari wake wamejipanga kisayansi ili kudhibiti uhalifu kwenye sikukuu ya Krisimasi na mwaka mpya 2020.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Desemba 24, 2019, Kasabago amesema watakaofanya uhalifu watachukuliwa hatua kali na askari polisi kwa kukamatwa na kulazwa mahabusu.

Amesema askari polisi wamejipanga kuhakikisha usalama wa raia unaendelea kuwapo katika mkoa huo kwa wananchi kusherehekea kwa amani.

Amesema askari polisi watakuwa kwenye doria, kwa miguu, magari, wakiwa na sare na wasiokuwa na sare ili kufanikisha ulinzi na usalama unakuwepo kwenye sikukuu hizo.

"Pia, natoa onyo kwa wenye kumiliki kumbi za starehe, endapo huna kibali cha kupiga disco toto usifanye hivyo na idadi ya watakaoingia iuwiane na nafasi iliyopo ili kusitokee madhara kwa watoto," amesema Kasabago.

Amewaasa wananchi wa mkoa huo kushiriki sikukuu ya Krisimasi na mwaka mpya wa 2020 kwa amani kwani mtu yeyote atakayesababisha vurugu au kufanya uhalifu Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, Zephania Chaula amesema atatumia sikukuu ya Krisimasi kwa kusherehekea na watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu kwenye tafrija iliyoandaliwa na mdau wa maendeleo wa mji mdogo wa Mirerani Charles Mnyalu.

Chaula amesema atashirikiana na viongozi wa eneo, wadau na watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi katika kusherehekea sikukuu hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz