Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Kyela wajipanga kukabiliana na vijana waliojiingiza kwenye uhalifu

Kyle Wizi Watototo Polisi.png Polisi Kyela wajipanga kukabiliana na vijana waliojiingiza kwenye uhalifu

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kyela, (Ocd) Lwitiko Mwanjala akizungumza na wananchi wa Kata ya Ndobo wakati akijibu malalamiko yao ya kukithiri kwa matukio ya uharifu. Picha na Hawa Mathias

Ni baada ya wananchi kulalamikia kukithiri kwa vitendo vya uharifu vinavyohusishwa na makundi ya watoto wanaodaiwa kuacha masomo na kuhusika na matukio hayo ikiwepo wizi wa mazao hususan kakao mashambani.

Kyela. Jeshi la Polisi Wilaya ya Kyela limesema linaanza oparesheni kapambe ya kukabiliana na makundi ya uharifu yanayohusisha vijana wenye umri mdogo katika vijiji vinavyozunguka Kata ya Ndobo Wilaya ya Kyela.

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kyela (OCD), Lwitiko Mwanjala amesema leo Jumanne Septemba 26, 2023 kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mbunge wa Kyela Ally Mlaghila, wenye lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuelekeza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020.

Mwanjala amesema kuwa kufuatia kuripotiwa kwa matukio mbalimbali ya kiharifu, Mbunge wa Kyela ametoa Sh 5 milioni kwa ajili ya ukarabati wa magari na ununuzi mafuta sambamba na matairi nane ambapo kila moja lina thamani ya Sh1.3 milioni.

Aidha amesema Jeshi la Polisi halitoshindwa kudhibiti waharifu na lipo kwa ajili ya kulinda amani na kuonya kikundi kinachojihusisha na uharifu wa kudhuru watu na kuiba kakao mashambai kuwa hawatafumbiwa macho.

“Leo tutaleta Askari hapa kwa ajili ya msako wa waharifu na wataobainika watawajibishwa kwa mujibu wa sheria ,pia tuwatake wananchi kutoa ushirikiano wa kuwafichua,”amesema.

Amesema Serikali ya awamu ya sita inataka watanzania wawe salama na mali zao sasa inapojitokeza kundi la watu wachache kuvuruga amani halikubaliki.

Awali, Anastazia Kyusa alimueleza Mbunge wa Kyela, Ally Mlaghila kuwa wamekuwa wakikosa usingizi na idadi kubwa walengwa wa matukio ya uharifu ni vijana wanaoishi kijijini hapa ambao wameacha masomo.

“Mbunge wananchi hatulali tunamulikwa na matochi tukiwa tumelala usiku na wezi, kuna watu wanapigwa na kufa na makundi ya vijana watu ambao wameacha masomo na kujihusisha na uharifu,”amesema Edward Mwafulila.

Amesema hali ya usalama kwao ni ndogo huku maisha yao yakiwa mashakani na kuomba Jeshi la Polisi kuimarisha doria za mara kwa mara ili kuokoa uhai na mali zao.

Naye, Tukuswiga Mwakyoma amesema mbali na watu kivamiwa, wizi wa mazao pia kumekuwepo na matukio ya watu kubakwa, hali ambayo imejenga hofu kuwatuma watoto nyakati za jioni kufanya mahitaji.

Mbunge wa Kyela, Ally Jumbe amewataka vijana kuepuka kutumika na badala yake waunge mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita kuwekeza kwenye kilimo.

“Vijana acheni kutumia Serikali inaleta fursa nyingi za kujiajiri na pia kuahidi kushughulikia suala la walimu wa shule za sekondari ambao wanawaelekeza wazazi ambao watoto wao hawataki elimu kuandika barua hali ambayo inachangia kuwepo na kundi kubwa la vijana wasio na ajira,”amesema.

Ameongeza kuwa, “Nimesikia kuna Mwananchi amelakamikia hilo kweli wema wote wa Rais Samia Suluhu Hassan kutoa elimu bure kuanzia awali, msingi na Sekondari wapo walimu wanaokubaliana na wazazi watoto kuacha masomo kwa maandishi hilo lazima lishughulikiwe,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live