Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Kiteto yanasa kilo 150 za mirungi

Vijiji Vitatu Vyaacha Kulima Mirungi Same.png Polisi Kiteto yanasa kilo 150 za mirungi

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi wilayani hapa, mkoani Manyara, limekamata dawa za kulevya aina ya mirungi bunda 230 sawa na kilo 150 zilizokuwa zinasafirishwa.

Watuhumiwa baada ya kuona Polisi wametelekeza pilipiki zao mbili zilizotumika kubebea dawa hizo.

Hayo yamesemwa leo Novemba 21 na Kamanda wa Jeshi la Polisi Kiteto, ACP George Katabazi.

"Saa 10 alfajiri kuamkia Septemba 21, 2023 maeneo ya pori namba mbili, Kijiji cha Kimana, kata ya Partimbo, tarafa ya Kibaya wilayani Kiteto mkoani Manyara, Askari Polisi waliokuwa kwenye doria wamekamata mirungi bunda 230 zenye uzito wa kilo 150 zikiwa zinasafishwa kwenye pikipiki mbili ,"amesema Kamanda Katabazi.

Amesema pikipiki hizo zilikuwa aina ya Tbetter rangi nyekundu na Sinoray rangi nyeusi, watuhumiwa walikimbilia porini walipokuwa wanakabiliana na Jeshi la Polisi.

“Jeshi la Polisi Manyara tutaendelea kuwasaka wahalifu hawa mpaka watakapopatikana kwani wanafahamika wao na vyombo vyao vya usafiri, hivyo ni rahisi kuwatia nguvuni ila nitoe rai kwao wafike kituo cha Polisi tu kujisalimisha na hata kama hawatajisalimisha sisi tutawakamata na kuwafikisha mahakamani"amesema ACP Katabazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live