Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Kilimanjaro waimarisha ulinzi sikukuu

Newslite Maigwa Polisi Kilimanjaro waimarisha ulinzi sikukuu

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa amesema kuelekea sikukuu za Krismasi na mwaka mpya watoto katika mkoa huo wataruhusiwa kwenda kwenye maeneo ya wazi kusherehekea mchana huku akisisitiza kuwa saa 12 jioni wahakikishe wamerejea majumbani

Kamanda Maigwa amewataka wazazi kuwa waangalifu wanapotoka na watoto hasa katika maeneo yenye vilevi na mchanganyiko wa watu kwani sio salama kwa watoto hao.

Ameeleza kuwa Jeshi la Polisi Kilimanjaro limejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa mkoa huo unakuwa na ulinzi wa kutosha katika kipindi hiki huku akitoa onyo kali kwa madereva wazembe na wanaotumia vilevi kuacha tabia hiyo kwani husababisha ajali zinazoepukika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live