Sun, 13 Aug 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Jeshi la Polisi Tanzania limekanusha ujumbe unaosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu mauaji ya Askari na Raia Kibiti.
Taarifa iliyotolewa leo na Jeshi la Polisi inaeleza kuwa hakuna matukio kama hayo, Kibiti ni shwari na salama hivyo ujumbe huo unapaswa kupuuzwa, sambamba na watu wasioitakia mema nchi wapuuzwe.
“Puuzeni uzushi huu, pia endeleeni kuwapuuza wasioitakia mema Nchi yetu,” imesema taarifa hiyo.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live