Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Katavi yajidhatiti kukabiliana na wahalifu

Polisi Katavi Dvf Polisi Katavi yajidhatiti kukabiliana na wahalifu

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi limefanya matembezi ya kijeshi ili kujiweka tayari kukabiliana na uhalifu wa aina yeyote unaotokea ndani ya mkoa wa Katavi.

Polisi imewataka wananchi kufichua kundi la watu wanaojiita damu chafu wanaojihusisha na uhalifu wa kupora na kujeruhi watu kwa kutumia vitu vyenye ncha kali hasa nyakati za usiku.

Elimu hiyo imetolewa na jeshi la polisi akiwemo Kamanda wa jeshi hilo Kaster Ngonyani katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Mpanda kama vile sokoni na maeneo mengine yenye mikusanyiko ya watu.

Wakati utayari huo ukiendelea wananchi walipaza sauti zao wakionyesha kuchoshwa na vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na kikundi cha damu chafu.

Aidha jeshi la polisi mkoa wa Katavi liliwataka madereva wa vyombo vya moto kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live