Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi: Hali ni shwari ziwa victoria

Maafisa Wa Polisi Watoweka Baada Ya Boti Kuzama Katika Ziwa Victoria Polisi: Hali ni shwari ziwa victoria

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

IMEELEZWA kuwa hali ya ulinzi na usalama ndani ya ziwa Victoria inaendelea kuimarika tofauti na miaka ya nyuma kutokana na tathimini zilizofanyika kupitia vikao vitano vilivyohusisha Maofisa wa Jeshi la Polisi, maafisa uvuvi pamoja na taasisi nyingine zinazohusika na ulinzi wa rasilimali ndani ya ziwa hilo.

Taarifa hiyo imetolewa Oktoba18, 2023, na Mkuu wa Usimamizi wa Vikosi Maalum vya Polisi kutoka Kamisheni ya Opereseheni na Mafunzo, Makao Makuu ya Polisi Dodoma (DCP), Ferdinand Mtui katika kikao maalum kilichowakutanisha Makamanda wa Jeshi la Polisi kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa na wadau wa uvuvi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Operesheni za Jeshi la Polisi Nchini, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Mihayo Msikhela amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2019-2020 kuliibuka uhalifu ndani ya ziwa Victoria ikiwemo mauaji, unyang'anyi wa kutumia silaha, uporaji wa nyavu, samaki na boti za Injini.

SACP Mihayo aliongeza kuwa vitendo hivyo vilipelekea majeruhi na vifo kwa baadhi ya wavuvi na wafanyabiashara ziwani lakini kwa sasa matukio hayo yamedhibitiwa kwa kiasi kikubwa. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live