Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Dar yatoa masharti kufanyika disko toto Krismasi

89374 Disko+pic Polisi Dar yatoa masharti kufanyika disko toto Krismasi

Fri, 20 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Kuelekea sikukuu za Krismasi na mwaka mpya 2020, Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam nchini Tanzania imepiga marufuku disko toto katika kumbi zote za starehe.

Pia, jeshi hilo limewaasa wananchi kusherekea kwa amani na utulivu na kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa sheria wakati wote wa sikukuu hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Desemba 20, 2019 Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limejipanga kukamilifu kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa kipindi chote cha sikukuu.

"Jeshi la polisi linakataza mikusanyiko pamoja na disko toto katika kumbi zote za starehe hadi zitakapokaguliwa na ofisa utamaduni na kupewa kibali," amesema Mambosasa

"Kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, tunawahakikishia wananchi tumejipanga kikamilifu kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa kipindi cha sikukuu za Krismasi na mwaka mpya 2020," amesema

Aidha Mambosasa amesema doria zitaimarishwa maeneo yote yenye mikusanyiko ya watu ikiwa ni pamoja na fukwe za bahari, nyumba za ibada na kumbi zote za starehe.

"Tunawatahadharisha wote wanaoendesha vyombo vya moto kufuata sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuepuka kujaza watu kupita kiasi, kubeba mishikaki kwenye pikipiki, kuendesha wakiwa wamelewa na mwendo wa kasi," amesema

Ameongeza kuwa jeshi hilo halitasita  kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaokiuka sheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha Mahakamani.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz