Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi DAR yatenga mil2/- kubaini majambazi

3b926e5bcb6b5b4d0c3f436bb5c25d31 Polisi DAR yatenga mil2/- kubaini majambazi

Wed, 23 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

JESHI la Polisi Kamanda Maalum ya Dar es Salaam limetangaza kutoa zawadi ya Shilingi milioni mbili kwa raia atakayetoa taarifa sahihi za mhalifu akiwa na silaha hasa bunduki.

Kamanda wa polisi Kanda hiyo Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Muliro Muliro amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Kamanda Muliro amesema jeshi hilo litahakikisha siri za mtoa taarifa zinatunzwa kwa kiwango cha juu na bila kuathiri mazingira ya usalama wake.

Amesema zawadi hizo zitaanza kutolewa bila kuzungushwa ili mradi vigezo vilivyotajwa vinazingatiwa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz